» »Unlabelled » AUDIO: Promota Siraji kasimulia kifo cha Bondia Thomas Mashali kilivyotokea

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Leo October 31 2016 zimeripotiwa taarifa za kifo cha Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Tanzania, Thomas Mashali ambapo imeelezwa Marehemu Mashali alifariki usiku wa kuamkia leo maeneo ya Kimara Dar es salaam kwa kushambuliwa na watu baada ya kusingiziwa ni mwizi na watu ambao aligombana nao.

Promota Siraji Kaike amesimulia tukio lilivyokua kwa kusema >>>’Alitoka kikaoni akaenda kimara kwa rafiki yake alipofika kule jamaa wakamshawishi  akanywa bia kidogo baadaye wakahamia sijui baa gani ambapo waligombana na jamaa, na Mashali huwa anakuwa mtemi akilewa, jamaa wakamuitia mwizi wakampiga mapanga’

>>>’Baadae wanagundua sio mwizi tayari washampasua alama kubwa sana na tayari alikuwa ameshapungukiwa na damu nyingi sana wakawa wamemtupa baada ya hapo bodaboda walikuwa wanamjua Thomas wakamuokota na kumpeleka hospitali, mdogo wake alienda muhimbili akapewa taarifa kuwa amefariki’ – Siraji


ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post