» »Unlabelled » Abiria wa Ndege walazimishwa kupima uzani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Shirika la Ndege limewataka abiria wake kupima uzani

Shirika moja la ndege Marekani limelalamikiwa na wateja wake kwa kuwalazimisha kupima uzani kabla ya kuingia ndani ya ndege zao. Lalama hizo zimetolewa na wafanyibiashara wawili kutoka Kisiwa cha American Samoa.

Wawili hao wameambia Mamlaka ya uchukuzi nchini Marekani kwamba walilazimishwa kupima uzani wao wakati wakianza safari yao kutoka mji wa Honolulu. Kituo cha Radio nchini New Zealand kimesema raia hao walikerwa sana waliponyimwa haki ya kuchagua viti vyao kwenye ndege kutokana na uzani wao. Walikua wakitoka Kisiwani Hawaii kuelekea mji wa Pago Pago.

Masharti ya abiria kupima uzani yamewekewa raia wa Kisiwa cha America Samoa, baada ya Kisiwa hicho kutajwa kuongoza kuwa na watu wanene kupindukia duniani

Raia wa kisiwa hicho kilichoko Bahari ya Pacific wameripotiwa kupenda vyakula vyenye mafuta mengi na hawafuati lishe bora. Mtu mmoja kati ya watu watatu anaugua kisukari katika Kisiwa cha American Samoa. Kwa sasa mamlaka ya uchukuzi Marekani imesema inachunguza lalama za wafanyibiashara hao.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post