» »Unlabelled » Wazee nchini wakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Imeelezwa kuwa wazee nchini wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na kutokuwa na nguvu ya kutumika kwa shughuli za kujiongezea kipato.

Hatma ya hali hiyo inategemea utashi wa serikali katika kutunga sheria ya usimamizi wa masuala ya wazee ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa takribani miaka kumi na tatu sasa.

Mtetezi wa haki za wazee kutoka mkoani Morogoro mzee Samson Msemembo amesema hayo leo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi ya HelpAge International ofisi ya Tanzania, kuhusu namna wanahabari wanavyoweza kutumia taaluma yao kupaza sauti juu ya hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili wazee nchini.

Kauli ya Mzee Msemembo imeungwa mkono na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa HelpAge Tanzania Bw. Smart Daniel, ambaye amewatahadharisha vijana kuwa hali yao ya kiuchumi wakati wa uzee wao haipo salama hata kidogo iwapo usimamizi wa haki za wazee nchini utabaki ulivyo hivi sasa na kwamba kuna haja ya kuhakikisha nchi inakuwa na sheria ya wazee ambayo ndani yake kutakuwa na pensheni jamii itakayotolewa kwa wazee wote.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post