» »Unlabelled » Tanzania na Urusi zakubaliana kuimarisha mahusiano

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Popov, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo huku wakitilia mkazo katika kukuza biashara na uwekezaji.

Pamoja na hayo Balozi Yuri Popov amepongeza na kuelezea kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli katika kuimarisha uchumi huku akibainisha kuwa kwa hatua hizi anaamini ajenda ya kujenga uchumi wa viwanda itafanikiwa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea taarifa ya hali ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na katika mazungumzo yake na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele, amemtaka kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa maabara hiyo ili kuongeza ufanisi wa majukumu yake ambayo ni kufanyia uchunguzi vielelezo vya makosa ya Jinai na usimamizi wa sheria za udhibiti wa kemikali na udhibiti wa vinasaba vya binadamu (DNA).

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post