» »Unlabelled » Massauni azuia safari za mabasi mabovu Ubungo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuf Masaun leo amefanya ziara ya ghafla katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo na kufanya ukaguzi wa mabasi pamoja na kituo kidogo cha Maili Moja na kulazimika kusitisha safari za mabasi mawili kutokana

Baada ya kufika katika kituo cha Ubungo Mh. Masauni aliamuru basi la Shambalai linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Lushoto lenye namba za usajili T419 BUF, pamoja na basi la kampuni ya Karachani lenye namba za usajili T253 CLZ na kutaka yasitishe safari baada ya kutokidhi vigezo vya kusafirisha abiria.

Aidha Masauni ametoa wiki moja kwa maofisa wa usalama barabarani Mkoani Pwani kuhakikisha wanafanya mabadiliko ya ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha maili moja mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha kutetea abiria (CHAKUA) Bw. Hassan Mchanjama ameomba kuboreshwa kwa huduma katika kituo cha Ubungo ili kuendana na hadhi yake.

Katika ziara hiyo, Masauni aliongoza na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga .
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post