
Sergio Aguero
Aguero alimpiga kiwiko Winston Reid
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28,alizozana na Reid wakati wa ushindi wa 3-1 katika mechi ya ligi ya Uingereza.
Iwapo atapatikana na hatia ,mchezaji huyo wa Argentina atapigwa marufuku ya mechi tatu na kukosa deby ya Manchester mnamo tarehe 10 mwezi Septemba.
Pia ataikosa mechi ya ligi dhidi ya Bournemouth pamoja na ile ya kombe la EFL dhidi ya Swansea.
