Kamanda wa Polisi mkoani Njombe Pudensiana Protas
Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia vijana wawili wakazi wa mkoa jirani wa Iringa wakiwa na meno sita ya Tembo yenye uzito wa kilo 13.6 ambayo walikuwa katika harakati za kutafuta wateja.
Kamanda Protas amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Emanuel Lyabonga na Thomas Mhomba wakazi wa Iringa na kwamba wamekamatwa na jeshi hilo wakiwa na pikipiki yenye namba za usajili MC 916 AWN.
Kuhusu thamani ya meno hayo Protas amesema kuwa wanasubiri wataalamu kutoka Idara ya maliasili ili kutambua thamani yake huku akitoa wito.