» »Unlabelled » Mwanamke ashikwa na heroine kete 190

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Morogoro. Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwanamke mmoja Mwanahamisi Kachenje(42) mkazi wa Kingolwira kwa tuhuma za kukutwa na kete 190 za madawa ya kulevya aina ya heroine pamoja na puli moja la bangi zikiwa zimeviringishwa kwenye chandarua ndani ya nyumba yake.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonce Rwegasira amesema kuwa tukio hilo limetokea leo saa sita mchana huko eneo la Mwembemsata Kingolwira Wilaya ya Morogoro.

Rwegasira amesema askari wakiwa katika msako maalumu ikiwa ni utekelezaji wa vita dhidi ya madawa ya kulevya ndipo walipomkamata na kumpekua mtuhumiwa na baada ya kufanya upekuzi nyumbani walibaini kuwa amekuwa akihifadhi dawa hizo kwenye mfuko wa rambo wenye chandarua ndani ya chumba chake.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post