Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata afisa mkuu wa muungano wa wapiganaji wa uhuru alipokuwa akitoka mahakamani baada ya kusikiliza kesi ya mwenzake ambaye anakabiliwa na shtaka la kumtukana rais Robert Mugabe.
Victor Matemadanda ,katibu mkuu wa muungano wa wapiganaji wa uhuru nchini humo alikuwa afisa wa pili aliyekamatwa katika msako wa viongozi wa muungano huo.
Wiki iliopita bw Mugabe alisema kuwa wapiganaji wa kivita waliotoa taarifa iliomshtumu kwa kuwa dikteta watatajwa na kuadhibiwa.
Bw. Matemadanda atashtakiwa kwa kumtusi na kukandamiza mamlaka ya raia,alisema Irene Petras ,mkurugenzi wa mawakili wa haki za kibinaadamu nchini Zimbabwe.
Ni mashtaka kama hayo ambayo msemaji wa muungano huo Douglas Mahiya anakabiliwa nayo baada ya kukamatwa siku ya Jumatano,alinukuliwa akisema.