Jambo! Unaifahamu miji mizuri zaidi Tanzania?
Kadri muda unavyozidi kusonga mbele Tanzania yetu inazidi kupendeza. Biashara zinatanuka, wawekezaji wa ndani na nje wanaongezeka pia. Hali ya maisha nayo inakuwa bora zaidi. Leo, iringaonline.com tunaitizama miji 9 bomba zaidi inapohiska +255, Tanzania.
8. Iringa.
Wajerumani walijenga ngome ili kupambana na Chief Mkwawa. Ngome hii ilibatizwa kwa kihehe, “Lilinga”. Hii ndiyo Iringa ya leo. Afrika Mashariki nzima, Iringa ni moja wapo kati ya mikoa yenye hali ya hewa nzuri zaidi na ya kipekee. Iringa kuna fursa nyingi za kilimo na uwekezaji pia. Iringa inavutia sana, ina mbuga nyingi za wanyama, ina mito mingi ya kuvutia. IringaOnline.com tunaona fahari kuwa sehemu ya mkoa huu mzuri na wenye watu wakarimu. Kamwene!
7. Moshi
Massawe! Mbege! Moshi ni Pesa tu zinaongea, ofcourse na mbege kidogo. Huu ni mji msafi zaidi Tanzania. Moshi ni mji unaopatikana pembezoni mwa Mlima mrefu zaidi Afrika, Kilimanjaro. Fursa zimejaa Moshi. Hasa katika sekta ya utalii na biashara za jumla na rejareja.
6. Mbeya.
Hili ndilo jiji pekee linalopatikana ukanda wa kusini mwa Tanzania. Mbeya imezungukwa na milima, mabonde na mito ya kuvutia. Hali ya hewa ni nzuri na yenye ubaridi. Mbeya ni hazina ya rutuba. Fursa nyingi zipo katika kilimo. Mbeya ni fahari ya asili. Ukisikia Green City, ndiyo hapa. Jiji la kijani, asili.
5. Morogoro
Mji kasoro bahari. Morogoro ni moja wapo kati ya miji iliyochangamka zaidi Tanzania. Mji huu huchangamka sana nyakati za asubuhi na mchana hasa kutokana na huduma za usafirishaji zinazopita hapa. Morogoro inajivunia Mlima Uluguru na mbuga za wanyama kama Mikumi. Muonekano wa mji huu ni wa kuvutia sana kwa jinsi ulivyo wa asili. Kuna kilimo cha katani pembezoni mwa barabara kuu. Morogoro kuna sanaa za kutosha.
4. Dodoma
Idodomya! Jiji kuu la Tanzania. Dodoma ni mkoa unaopatikana katikati kabisa ya nchi. Dodoma ni jiji lililochelewa kukua, lakini kwa sasa kasi ya ukuaji wa jiji hili ni kubwa sana. Hali yake ya ukame na jua kali haivutii sana lakini bado ni sehemu nzuri sana ya kuishi na kutembelea. Fursa ni biashara na hali ya hewa inaruhusu kilimo cha zabibu zinazotumika kutengeneza mvinyo.
3. Arusha
Jiji hili linapatikana kaskazini mashariki mwa Tanzania. Arusha ni mkoa uliotulia. Unavutia sana watalii. Arusha kuna sehemu nyingi sana za utalii. Fursa zinazopatikana ni pamoja na Biashara, kilimo na shughuli za utalii. Ni moja wapo kati ya sehemu zinayovutia zaidi kuishi. Huduma zote zinapatikana, za kitaifa na kimataifa.
2. Mwanza
Rock City. Jiji lililopo kanda ya ziwa Victoria. Mwanza ni miongoni mwa majiji yanayokua kwa kasi zaidi Afrika. Mwanza imezungukwa na mawe makubwa. Fursa za kiuchumi ni nyingi sana. Inapakana na wilaya zenye madini mbalimbali ya thamani. Samaki aina ya Sato na Sangala wana umaarufu sana katika jiji hili. Kilimo cha mpunga na mahindi pamoja na shuguli za uvuvi ni aina ya biashara maarufu sana hapa.
1.Dar es Salaam
Dar es Salaam ni jiji linalokua kwa kasi ya ajabu kila kukicha. Huduma zote katika ngazi za kitaifa na kimataifa zinapatikana hapa. Mzunguko wa biashara ni mkubwa sana. Jiji hili lina sehemu nyingi za burudani na zenye kuvutia. Fursa kubwa ni biashara na ujasiriamali unaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jiji hili. Karibu, Tanzania.