Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mbeya baada ya kukamatwa akiwa amevalia sare za Jeshi la Wananchi sambamba na kukutwa na risasi 10 za bunduki aina ya SMG wakati sio askari,huku Jeshi hilo pia likifanikiwa kukamata bidhaa za aina mbalimbali zinazodhaniwa kuwa za wizi yakiwemo magari,bajaj,Computer na vitu vingine vya majumbani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi,Dhahir Athuman kidavashari amemtaja mtuhumiwa aliyekutwa na sare za jeshi la wananchi wa tanzania pamoja na risasi 10 zinazotumika kwenye bunduki aina ya SMG kuwa ni John Mwasumbwi ambaye alikamatwa baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa zake kutoka kwa wasamalia wema.
Mbali na tukio hilo,Kamanda Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Polisi limefanya msako mkali jijini Mbeya na kufanikiwa kukamata bidhaa mbali mbali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi,yakiwemo magari,pikipiki za magurudumu matatu maarufu kwa jina la bajaj,Coputer,Tv na bidhaa nyingine za madukani na majumbani,huku watu 10 wakitiwa mbaroni wakihusishwa na bidhaa hizo.
Kamanda Kidavashari amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuifanya Mbeya kuwa mahali salama pa kuishi,huku akiwaonya watu wanaojihusisha na wahalifu kuwa watafute kazi nyingine za kufanya kwa jeshi lake limejipanga kuwadhibiti.