» »Unlabelled » Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya tano imejikita kutoa miradi ya kazi za wahandisi wazawa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema serikali ya awamu ya tano imejikita kuhakikisha inatoa miradi ya kazi za wahandisi kwa wahandisi wazawa ili kuongeza ujuzi wa wahandisi wa ndani, huku ikitarajia kupata miundombinu bora na inayoonekana kwakuwa eneo la uhandisi katika nchi kwa upande wa ujenzi linajenga uchumi wa nchi na kukuza pato la mtu mmoja mmoja.

Makamu wa Rais ameyasema hayo katika kongamano la pili na maonesho la wahandisi wanawake nchini ambapo amesema lengo ni kuwawezesha wahandisi kuongeza ujuzi kwa kuwapatia fursa hivyo amewataka kuzidisha ushirikiano baina yao na kuwa walezi na walimu wa wasichana wadogo ili kuwahamasisha kuipenda na kutambua umuhimu wa taaluma hiyo katika nchi ili kuweza kuwa na uwiano mzuri wa wahandisi wanawake na wanaume.

Awali akizungumza katika kongamano hilo msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi Tanzania (ERB) Steven Mlote, amesema wahandisi wa kike ni mtaji kwa nchi, kwakuwa wapo makini kuzingatia weledi hivyo wakiwa wengi nchi itasonga mbele ambapo kwa sasa wapo asilimia nane tu kati ya wahandisi 17,122 huku wahandisi wanawake wabobevu wakiwa kumi na watatu tu.

Kufuatia umuhimu wa taaluma ya uhandisi Tanzania na duniani kwa ujumla, ubalozi wa Norway umekuwa msitari wa mbele kuisaidia serikali kuendeleza taaluma hiyo kwa miradi mbalimbali ikiwemo kudhamini kongamano na maonesho ya wahandisi wanawake na mnamo mwaka 2010 ilidhamini mradi wa Sh.bilioni tatu uliowaendeleza wahandisi wanawake 192, na mradi unaoendelea sasa wa miaka mitano 2016-2021 unaolenga kuwaendeleza wahandisi wanawake 150 katika masuala ya gesi na mafuta.

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post