Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga mzimbabwe, Donald Ngoma ataikosa mechi dhidi ya waarabu wa Algeria, MO Bejaia kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano ambapo kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mchezaji anapaswa kukosa mchezo unaofuata
Yanga ikiwa inatafuta ushindi kwa udi na uvumba katika mechi hiyo dhidi ya Mo Bejaia itamkosa mshambuliaji wake huyo aliyefunga mabao manne mpaka sasa katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kutokana na hilo, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema Ngoma ni mchezaji muhimu lakini kwa kuwa ana kikosi kipana hakuna tatizo katika hilo, ataiziba nafasi hiyo siku hiyo na kila kitu kitakwenda sawa.
Yanga inatarajia kuvaana na Bejaia Agosti 13, mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Katika mechi ya Bejaia nitamkosa Ngoma tu kutokana na kadi mbili za njano alizonazo, kweli ni mchezaji mzuri lakini kwa kuwa nina kikosi kipana hapa, hakuna kitakachoharibika, tutawatumia waliopo kwa ajili ya kuipigania timu,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi.
Katika michuano hiyo, hii ni mara ya pili, Ngoma anakaa nje kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano, awali alikosekana katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.