» »Unlabelled » Chadema Kanda ya Kusini kufanya mikutano 8,764

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Mtwara. Viongozi wa Chadema Kanda ya Kusini wameunga mkono maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema ya kufanya mikutano 8,764 na maandamano kupinga kinachoelezwa ni udikteta nchini.

Kanda hiyo inayojumuisha mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara imesema Operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Septemba Mosi inalenga kupinga viashiria vya udikteta vinavyoonyeshwa na serikali ya awamu ya tano.

Katibu wa Kanda hiyo, Philbert Ngatunga amesema maandalizi ya awali yameanza kufanyika na wanatarajia kila ngazi itafanya maandamano na mkutano mmoja na kufanya jumla ya jumla ya makundi ya maandamano na mikutano 8,764.

Ngatunga pia amelaani kauli ya msajili wa vyama vya siasa dhidi ya Chadema aliyoitoa kupitia vyombo vya habari Julai 27, kuwa mambo yote aliyoyasema hayapo.

Kauli hiyo inaunga mkono maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema katika kikao cha dharura cha Julai 23 hadi 26 mwaka huu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post