Mtu anayeaminika kuwa mashambuliaji amejisalimisha kwa polisi
Ripoti nchini Japan zinasema kuwa mtu mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi katika kituo hicho cha Tsukui Yamayuri-en, alijipeleka hadi kituo cha polisi na kukiri kuwa ndiye aliyetekeleza mauaji hayo ya kutisha na kwa sasa anazuiliwa.
Mtu huo ametambuliwa kama Satoshi Uematsu, mwenye umri wa miaka 26.
Polisi wanasema mshukiwa alikuwa amemwandikia barua spika wa bunge la chini mwezi Februari akitishia kuwaua walemavu.
Alitibiwa hospitali lakini baadaye akaachiliwa.
Visa vya mauaji ya watu wengi kwa pamoja huwa nadra sana nchini Japan.
Visa vya watu kuchomwa visu mwaka 2001 na 2008 vilisababisha vifo vya watu saba na wanane mtawalia.
Mwaka 1995, shambulio la kutumia gesi ya sumu ya sarin katika treni mjini Tokyo, ambalo lilitekelezwa na watu wa madhehebu ya Aum Shinrikyo, lilisababisha vifo vya watu 12.

