Katibu wa Idara ya Barabara kutoka Chama cha Kutetea Abiria(Chakua), Godwin Ntongeji alisema mabasi yalitakiwa kuanza safari zake saa 12:00 asubuhi kwa mujibu wa ratiba za Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra).
“Tangu saa 12 asubuhi abiria wamekwama kuondoka , yapo ambayo yanaendelea kufanyiwa matengenezo ili yaondoka, ukaguzi umeongezeka kwa sasa lakini abiria wanaumizwa sana kwani haiwezekani wakala wa basi akatishe tiketi kumbe basi bovu,”alisema huku akiwa amezungukwa na abiria wanaohitaji msaada kutoka ofisi yake.
Gazeti hili limeshuhusia baadhi ya mabasi hayo yakiwa yanafanyiwa matengenezo huku abiria wakilanda landa na wengine wakihitaji msaada wa mamlaka husika.
