Ajali hiyo iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni hiyo, moja likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyanga na lingine likitokea Kahama mkoani Shinyanga kuelekea Dar es
Salaam.
Tukio hilo lilitokea saa tisa jana katika eneo la Maweni, Kata ya
Kintiku, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Akizungumza leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Said
Mussa amesema katika ajali hiyo amempoteza baba yake mdogo Sinto na mkewe Rose na mtoto wao mdogo.
“Walifunga harusi mkoani Mbeya ukweni kwa hiyo walikuwa wakitoka kujitambulisha nyumbani kwa baba mdogo mkoani Tabora,”amesema Mussa.
