» » Wakazi Tabora wamlilia Mkuu wa mkoa kutohamishwa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Tukutuku Mjini Tabora wanaodaiwa kuvamia na kujenga eneo la shule ya wasichana ya Tabora, wamemuomba Mkuu wa Mkoa huo Aggrey Mwanri asitishe amri aliyoitoa ya kuwaondoa katika eneo hilo ndani ya siku 30.

Wakazi hao wamedai kuwa wakati wanajenga nyumba zao katika eneo hilo hawakujua kama ni la shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora na kwamba kwa sasa hawana mahali pa kwenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, amesema wananchi hao ni wavamizi hivyo ni lazima waondoke huku mwanasheria wa serikali ya Mkoa akiwataka wananchi hao kutii sheria za nchi.

Akizungumzia suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, amesema hatabadilisha kauli yake mpaka pale wananchi hao watakapokuja na vielelezo vyote vinavyoonyeshwa kukabidhiwa maeneo hayo kihalali na Manispaa ili achuke hatua zaidi dhidi ya watumishi waliowapa viwanja hivyo.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post