» » Bi Cheka arudi upya kwa kishindo

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

BAADA ya kimya cha muda mrefu msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, aliyewahi kutamba akiwa ndani ya Kundi la Wanaume Familiy, Cheka Haji ‘Bi cheka’ ameibuka upya kwenye tasnia hiyo baada ya kutoa ngoma kali inayokwenda kwa jina la Mapenzi ya Kale Siku Hizi Hakunaga aliyomshirikisha mkali kwenye gemu la Muziki wa Singeli, Marick Thadei ‘DJ Mack’.

Akichonga na Uwazi Showbiz, kwa niaba ya Bi Cheka, DJ Mack amesema wimbo huo umepikwa na prodyuza kutoka Natal Records aitwaye G Max na anaamini utafanya vizuri  hata kumrudishia Bi Cheka mashabiki waliokuwa wanamfuatilia.

“Wimbo ni mzuri kiukweli, ninatumaini utafanya vizuri na kumrudisha Bi Cheka kwenye reli maana ni kimya sasa kimepita tangu asikike kutokana na matatizo ya hapa na pale yanayoweza kumpata binadamu yeyote,” alisema DJ Mack.

Source: Global Publisher
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post