Hayati Bob Marley alirekodi takriban album 13 kuanzia mwaka 1965. Ajabu ni kwamba ukisikiliza wimbo wa kwanza katika album yake ya kwanza, The Wailing Wailers hadi wa mwisho kwenye album yake ya mwisho, Confrontation (1983), hakuna wimbo unaofanana na mwingine – kila moja imepita kwenye njia yake.
Ni kitu ambacho hadi leo huwa najiuliza Bob aliwezaje kuwa na nyimbo nyingi kama hizo lakini asizifananishe hata kidogo licha ya kwamba nyingi aliziandika mwenyewe!
Bob si msanii pekee duniani aliyekuwa na uwezo huo. Wasanii wengi wakubwa wamekuwa na uwezo wa kuukwepa mtego huu wa kufananisha nyimbo zao kwa kutumia waandishi tofauti tofauti.
Lakini kuna tatizo kubwa sana kwa sasa kwa waimbaji wengi wa Bongo Flava la kufananisha melody zao. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba wapo wale ambao kwenye kila wimbo lazima kuwe na kisauti fulani ambacho alikitumia kwenye nyimbo zake zilizopita. Kiukweli inachosha kumsikia msanii akiwa anaimba remix za nyimbo zake kila siku.
Kinachobadilika kwa waimbaji wa aina hii ni jina la wimbo, mashairi, lakini melody zinacheza kwenye funguo au chords zile zile. Madhara ya wasanii wa aina hii ni kuwa nyimbo zao haziwezi kudumu kama wataepuka wao wenyewe kupotea kabisa kwenye ramani kwa watu kuwachoka haraka.
Ni kwasababu udhaifu huu huwafanya wapenzi wa muziki wasiwe na hamu ya kusikiliza nyimbo zao mpya kwa matarajio kuwa hakuna kipya masikio yao yatapewa.
Tatizo hili linaweza kuepukwa kwa kufanya haya:
Kukubali kuandikiwa
Ni wasanii wachache sana wa Bongo Flava wanaoweza kukubali kujishusha na kumpa mtu mwingine kazi ya kumwandikia wimbo – wengi huona kama wanajidhalilisha ama mashabiki watawaona hawawezi. Lakini wale wanaotambua kuwa huo ndio mfumo unaotumika kwenye industry za wenzetu, wanaona matunda yake. Sio wasanii wote wenye uwezo wa kuandika nyimbo 10 zisizofanana na kama wanataka kuendelea kuwa ‘relevant’ hawana budi kufanya hivyo.
Ben Pol anafahamika kama mmoja wa waimbaji bora kabisa wa R&B nchini lakini aliamua kujishusha na kuandikiwa wimbo wake ‘Moyo Mashine’ ambao hadi leo umekuwa wimbo wake uliofanikiwa zaidi. Kitu kizuri kuhusu kuandikiwa ni kuwa mashabiki hawana habari ya nani aliyeuandika, wanachojali ni nani aliyeuimba. Shaa, Vanessa Mdee ni miongoni mwa waimbaji wanaoheshimu vipaji vya wengine na kuamua ‘kuazima jani’ kuboresha kazi zao.
Rihanna, Beyonce wapo hapo si kwasababu ni waandishi wazuri, bali ni waimbaji na watumbuizaji wazuri. Asilimia kubwa za kazi zao zimeandikwa na watu wengine ambao hakuna aliye na habari hata ya kutaka kuwajua majina yao.
Kutumia watayarishaji tofauti
Wakati mwingine tatizo la kufananisha melody huchangiwa na watayarishaji wa muziki. Pale msanii anapomtumia producer yule yule kwenye nyimbo zake zote, kuna sehemu nyimbo zitafanana tu. Hivyo wasanii wanapaswa kubadilisha watayarishaji ili kutengeneza taste zinazotofautina.
Kuomba ushauri
Wasanii wana kasumba ya kurekodi nyimbo nyingi. Lakini wapo ambao huchagua kutoa nyimbo wanazozipenda wenyewe bila kuomba ushauri kwa watu wengine. Wakati mwingine ni ngumu kwa msanii mwenyewe kujua mfanano baina ya nyimbo zake hadi pale anapohusisha sikio la mtu mwingine.
Kuongeza elimu ya muziki
Wasanii wengi wa Bongo Flava wanaimba kwa vipaji tu. Ukimuuliza anaimba kwenye key gani hawezi hata kukuambia – hajui, japo hilo si kosa. Lakini wasanii wa mbele kama Beyonce, Alicia Keys wanajua mambo haya hivyo ni rahisi sana kusikia mfanano wa nyimbo zake kwakuwa wana elimu hiyo tayari. Kwa wasanii wanaoimba kwa kubahatisha ni mtihani. Muziki ni kazi na kama ni kitu kinachokupa fedha kwanini usitafute muda wa ziada kujifunza kutoka kwa wataalam wa muziki ili kujiimarisha zaidi?
Kuwa na desturi ya kusikiliza muziki wa aina nyingi
Unaweza kuwa na utajiri mkubwa wa sauti iwapo unasikiliza muziki wa aina moja? Ni ngumu! Wasanii wanapaswa kuwa na desturi ya kuchimba na kusikiliza aina nyingi za muziki duniani. Jazz, R&B, muziki wa kihindi, kiarabu na ladha zingine zinaweza kukupa inspiration nyingi za kutofautisha sauti zako.