» » Tanzania ndani ya nne bora za China

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Dar es Salaam. Tanzania ni kati ya nchi nne ambazo Serikali ya China imeahidi kufanya ‘kufuru’ ya uwekezaji wa viwanda.

 Hayo yamebainika  kwenye kongamano la wachumi na wadau wa biashara kati ya China na Tanzania, Kenya na Afrika Kusini ambalo lilijadili fursa na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, ambaye alikuwa anafungua kongamano hilo, amesema uamuzi wa kuiteua Tanzania ulifanywa kwenye mkutano uliofanyika mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Amesema katika mkutano huo ambao Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, China iliamua kushirikiana na nchi za Afrika Kusini, Kenya na Tanzania kujenga uchumi wa viwanda.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post