» » Sigara na Mshumaa vyasababisha mabanda 500 kuteketea

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.

Sengerema, Mwanza
KATIKA matukio mawili tofauti moto umeteketeza vibanda zaidi ya  500 vya biashara visiwani Kabiga na Migongo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema leo kuwa katika Kisiwa cha Kabiga Kata ya Maisome zaidi ya vibanda 300 viliteketea Alhamisi wakati wafanyabiashara walipokuwa wakigawana mafuta ya petroli yanayodaiwa kuibwa.

Amesema mmoja wa wafanyabiashara hao aliagusha kipande cha sigara kilichowashwa ndipo moto ulipolipuka. Amesema katika Kisiwa cha Migongo Kata ya Maisome, zaidi ya vibanda 200 viliteketea jana usiku chanzo kikiwa ni mshumaa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post