» » Picha: Huyu ndiyo muuaji wa polisi watano huko Marekani

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Johnson akiwa kwenye sare zake za jeshi
 Muuaji wa polisi watano huko Dallas, Micah Xavier Johnson aliwahi kuwa muajiriwa wa jeshi la Marekani.

Johnson (25) alifanya tukio hilo la mauaji ya polisi watano na kujeruhi wengine 12 siku ya Jumatano baada ya polisi wa kizungu Jumanne hii kuwaua watu weusi wawili katika matukio tofauti akiwemo Philando Castile aliyeuwa akiwa kwenye gari huko Minnesota na Alton Sterling Louisiana aliyeuawa wakati akiuza CD kwenye eneo la kuegesha magari.
 Bunduki iliyotumiwa na marehemu Johnson kuwauwa polisi watano

Imedaiwa kuwa Johnson alitumia silaha aina ya AR-15 kwenye kutekeleza mauaji hayo ambapo alijificha karibia na chuo cha El Centro ambapo ambapo polisi hao watano walipoteza maisha akiwemo Patrick Zamarripa, Michael Krol, Lorne Ahrens and Michael J. Smith na Brent Thompson.
Micah Johnson akiwa na kaka yake, Tevin pamoja na dada yake Nicole

Afisa wa polisi wa Dallas, David Brown alisema, “The suspect said he was upset with white people and wanted to kill white people, especially white officers. We believe now that the city is safe, and we can move on to healing.”

Hata hivyo baada ya kufanya mauaji hayo ya polisi walifanikiwa kumuua Johnson. 
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post