Msanii 20% akiwa na Man Water
20% alisema hayo kupitia kipindi cha #eNEWS na kudai kuwa wasanii wasio na uwezo wa kutunga mashairi yenye tija kwa jamii wengi wao hawajafurahi kwani wanafahamu muungano wake na Man Water utaleta vumbi kwenye kazi zao.
"Kwanza naomba nikubaliane na wewe kwamba kitendo cha mimi kushinda tuzo tano mwaka 2011 kilikuwa chanzo cha mimi kushindwa kuji-control katika kipindi hicho na kupelekea ukimya wake katika soko la muziki" alisema 20%
Msanii huyo alizidi kutoa ufafanuzi kuwa "Baada ya mimi kushinda tuzo zile kila mtu na kila jambo lilielekezwa kwangu. Lakini nikwambie tu kuna mwanamuziki ambaye hana uwezo wa kuandika mashairi kama 20% hawezi kufurahia muungano kati yangu na Man Water kwa sababu anajua tayari balaa limeshaanza, vumbi linakuja, kwa hiyo huyo huyo msanii alikuwa ana support ugomvi kati ya 20% na Man Water" alisema 20%
