» » Ney wa Mitego aingiwa na hofu ya kufungiwa wimbo wake

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Msanii Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Saka hela' ameonyesha wasiwasi na kuhofia wimbo wake mpya ambao utatoka siku ya Jumatatu ya tarehe 11 kufungiwa.

Nay wa Mitego amesema wimbo huo 'Pale kati patamu' anaamini utachafua hali ya hewa tena kwa mashabiki kutokana na kile alichokiimba ndani ya wimbo huo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego alisema kuwa akisikiliza wimbo huo yeye mwenyewe anapagawa yaani, na kuwataka mashabiki kushika hiyo tarehe kwani watathibitisha wenyewe.

"Zimebaki siku kadhaa tu, Jumatatu Tarehe 11. Nitakua naachi wimbo wangu mpya. 'Pale kati Patamu' hii ngoma daaah mpaka napagawa yani. Shika iyo Tarehe na siku pale kati patamu sijui wataleta zengwe na hii?" aliuliza Nay wa Mitego

Nay wa Mitego kabla ya kuachia wimbo wake wa Saka hela, alitoa wimbo uliokuwa unafahamika kama 'Shika adabu yako' ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post