» » ‘Naagiza Mawaziri wote kuhamia Dodoma mara moja’-Waziri mkuu Majaliwa

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO



Kila ifikapo July 25 ya kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya mashujaa ikiwa kwa mara ya kwanza July 25 2016 maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika mkoa wa Dodoma ambapo pia mgeni rasmi alikuwa Rais John Pombe Magufuli akisindikizwa na viongozi wengine akiwemo Waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Majaliwa alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi ambapo moja ya sentensi zake ilikuwa ni agizo alililitoa kwa mawaziri wote kuhamia Dodoma ikiwa ni kuanza kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli kutaka serikali kuhamia mkoani humo.

‘Natoa maagizo kwa mawaziri wote wahakikishe wanahamia mara moja Dodoma kwakuwa najua wana nyumba za kuishi hapa lakini pia nimetoa maagizo nyumba yangu imaliziwe nitahamia Dodoma mwezi wa tisa mwaka huu ‘ –Waziri mkuu Kassim Majaliwa

‘Sasa huu ndio wakati wenu Dodoma kujiandaa kwani hizi ni fursa za kukamata pindi serikali ikihamia hapa‘ – Waziri mkuu Kassim Majaliwa
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post