» » Msichana amnyonga na kumtupa mtoni mtoto wake ili aolewe

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Msichana wa miaka 17 mkazi wa Makete mkoani Njombe Vumilia Kyando ambaye ni muhudumu wa baa amemnyonga na kumtumbukiza kwenye mto mtoto wake wa kumzaa John Kyando mwenye miaka miwili baada ya kupata mchumba ambaye si baba wa mtoto huyo aliyetaka kuishi nae lakini  akawa hamtaki mtoto huyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa  Njombe Kamishna Masidizi wa Polisi Podinsiana Protas ameiambia ITV kuwa Vumilia Kyando aliamua kumuua mwanaye wa kumzaa baada ya kumpata mwanaume aliyetaka kuishi nae lakini akawa hamtaki mtoto wa msichana huyo.

Kamanda Podinsiana Protas amesemna kuwa mwanamke huyo anahojiwa na polisi na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani huku wananchi mkoani Njombe wasikitishwa tukio hilo la mama kumuua mtoto wake wa kumzaa.

Katika tukio jingine mtoto wa miezi kumi na mbili Samweli Ahidimiwe ameuawa kwa kukatwa na jembe na Frola Sanga mkazi wa kijiji cha Kisaula wilayani Makete mkoani Njombe katika ugomvi wa kugombea mashamba ambapo Frola Sanga alikuwa akitaka kumkata kwa jembe bibi wa mtoto huyo Tulamba Konga ndipo akamuua kwa jembe mtoto huyo aliyebebwa mgongoni na bibi yake.


Upelelezi utapokamilika mtuhumiwa Frola Sanga atafikishwa mahakamani kwa kesi ya mauaji ya mtoto Ahimidiwe Sanga.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post