» » Ewura yapewa rungu jingine

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati, Maji na Mafuta (Ewura) itasimamia bei nishati hiyo.

Akifungua Kongamano la Tatu la Wadau Gesi ya Kupikia (LPG) barani Afrika, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo amesema mpango huo utaanza kutekelezwa Septemba.

“Changamoto iliyopo ni gharama kubwa. Uagizaji wa pamoja utashusha bei na kila Mtanzania atamudu. Hii itasaidia kuokoa misitu  kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa,” amesema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ununuzi wa Pamoja Mafuta na Bidhaa zake (PBPA), Michael Mjinja amesema jukumu lililo mbele yake ni kuisimamia sekta hiyo ili iwe na manufaa kwa kila mwananchi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post