MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo kali na kukiagiza Kituo cha Televisheni cha Clouds kuomba radhi wananchi kwa siku tano mfululizo kuanzia jana, baada ya kurusha mada inayohusu ushoga kupitia kipindi cha Take One.
Adhabu hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamati ya Maudhui ya TCRA iliyokuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Joseph Mapunda.
Akisoma uamuzi wa kamati hiyo, Mapunda alisema Clouds inatakiwa kuwaomba radhi watazamaji na watanzania kwa ujumla kila siku kuanzia jana katika taarifa ya habari ya saa 1:30 usiku na saa 5:00 usiku kutokana na kuwakwaza pamoja na kusababisha usumbufu kwa kurusha mada inayozungumzia ushoga kwa namna ya upotoshaji.
Alisema kamati imebaini kuwa kipindi hicho kilikuwa na majadiliano ya undani kuhusu ushoga, kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kitanzania, maswali mengi ya mtangazaji yalilenga kuhamasisha ushoga, ikiwa ni pamoja na matumizi ya lugha isiyo na staha na pia kipindi kutozingatia unyeti wa masuala ya ushoga na ngono na madhara yake kwa jamii.
“Katika mahojiano hayo, kijana aliyehojiwa alielezea kutojutia kuwa shoga na kuwa kuna faida anazozipata. Kutangaza taarifa kuhusu mapenzi ya jinsi moja huku shoga mtajwa akiwa mhusika na kupewa nafasi ya kujieleza waziwazi na kutoa nafasi ya uwezekano wa kutoa ushawishi kwa jamii ni ukiukwaji wa kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) za mwaka 2005 kifungu cha 5 (b), 5(c), 5(d), 15(c) na 16(2),” alisema.
Katika utetezi wake, Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba alisema pamoja na kueleza kuwapo makosa ya uvunjifu wa kanuni, lakini jamii yote inakubaliana kuwa ushoga ni kitu kibaya na si kitu cha kuungwa mkono.
Hata akizungumza baada ya kutolewa maamuzi hayo, alisema wanakusudia kukata rufaa kupinga uamuzi huo kwa madai kuna maneno mengine hayakuwepo kwenye kipindi hicho kama ilivyodaiwa na kamati. Kipindi hicho kilichorushwa Juni 28 mwaka huu, kilizua mjadala miongoni mwa jamii wakiwamo wabunge ambao waliiomba serikali kukichukulia hatua kituo hicho.