» »Unlabelled » CCM yatisha kwa ulinzi Dodoma

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi, CCM ilifanya kikao kwenye jengo lake la makao makuu lijulikanalo kama ‘white house’ chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye sare.

Hali hiyo ilipelekea kama hauhisiki na kikao hicho kutokusogea eneo hilo wala kupenyeza katika maeneo hayo.

Mpaka sasa haijajulikana kama wameweka ulinzi huo kutokana na tishio la vijana wa Chadema (BAVICHA) au ni mabadiliko ya kawaida, kuamua kuweka ulinzi katika kikao hicho au ni polisi kuamua kujipanga kivingine kiulinzi.

Vile vile askari polisi, vikosi vya mbwa na maofisa usalama wa Taifa walionekana wakizunguka maeneo yote kulizunguka jengo hilo lililopo barabara kuu, katikati ya mji wa Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alitoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayeleta vurugu, akisema wamejiandaa vizuri kukabiliana nao.

CHANZO: MWANANCHI

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post