
Barakah akiwa na mtangazaji maarufu wa Classic 105, Maina Kageni
Hata hivyo uongozi wake wa zamani, Royal Nsyepa Ltd unaendelea kuhaha ukidai kuwa msanii wao amepokonywa. Ijumaa hii mkurugenzi wa kampuni hiyo, Mkala Fundikira alitoa malalamiko yake kwenye Instagram kuelezea kusikitiswa kwake.
“Nachukua fursa hii kulaani vikali kitendo cha wanaoitwa Rock star kutangaza wamemsainisha msanii Barakah da prince huku wakijua kuwa msanii huyo bado ana mkataba nasi Royal Nsyepa Ltd,” aliandika.
“Kwakuwa ni wao ndio walitufuata kutaka kununua mkataba wetu na Barakah da prince basi waache mambo ya kihuni wamalize mchakato wa kununua mkataba huo,” aliongeza.
Hata hivyo Fundikira ameomba radhi kwa kauli hiyo na kudai kuwa aliandika kwa jazba.
“Nachukua fursa hii kuwataka radhi wanaoitwa Rockstar 4000, jana nilirusha maelezo yakieleza kusikitishwa na kitendo chao cha kutangaza kumsainisha mkataba msanii Barakah da prince kabla ya kuhamisha umiliki wake toka Royal Nsyepa Ltd kwenda kwao, kitendo ambacho nilikiita cha kihuni,” anasema.
“Napenda kusema kuwa nilitumia maneno hayo kwa jazba na bila kushawishiwa na mtu nimeamua kuondoa kauli yangu hiyo na kuondoa maelezo yangu toka mtandaoni. Nasisitiza kuwa maneno hayo niliyasema kwa jazba na nawaomba radhi wahusika na waliobugudhiwa na kauli ile.”
“Baada ya kusema hayo nawategemea Rockstar 4000 wakubali kuhusika kwao na suala hili na kwa muda mwafaka wamalize uhamisho wa msanii husika.Mwisho napenda kusema mstaarabu akikosea huomba radhi!.”
Kampuni hiyo ilimchukua Barakah kutoka kwenye uongozi wake wa zamani, Tetemesha na kusababisha malumbano mengine kama haya.
Kwa upande wa Barakah, mambo yanazidi kumnyookea huku akiwa busy kuzunguka kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV jijini Nairobi kwaajili ya mahojiano.
Na bila kusahau, penzi lake na Naj limeendelea kushamiri. Picha kubwa akiwa na mrembo huyo imewekwa kwenye akaunti yake ya Instagram.
