» » Young Dee akiri alikuwa akitumia madawa ya kulevya, aomba radhi na kuahidi maisha mapya

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Rapper Young Dee hatimaye amethibitisha tetesi za miaka mingi kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya na kukiri kuwa ametumia kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Escape One jijini Dar es Salaam, rapper huyo amewaomba radhi watanzania kwa vitendo hivyo na kuahidi kubadilika.

Amedai kuwa ni marafiki ndio waliompoteza na kumuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Amesema amepewa ushauri nasaha na wataalam na kwamba ameachana na matumizi hayo.

Pia rapper huyo amerejea rasmi kwenye uongozi wake wa zamani, Million Dollar Boyz, MDB alioachana nao mwaka jana.

Young Dee na meneja wake Max Rioba

Kwa muda mrefu rapper huyo alikuwa akikanusha tetesi hizo.

Taarifa zaidi zitakuja punde.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post