» » J Plus na Inspekta Seba wakutanishwa tena kwenye filamu mpya ya ‘The Foundation’

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


 Staa wa filamu za mapigano Bongo, Sebastian Mwanangulo aka J Plus anatarajia kuachia filamu yake mpya ‘The Foundation’ mwezi Julai mwaka huu.

Filamu ya mwisho ya J Plus ilikuwa ni ‘Double J’ iliyotoka mwaka 2012 na tangu hapo amekuwa kimya. J Plus anatarajia kuachia filamu hiyo iliyowashirikisha mastaa kadhaa akiwemo Inspekta Seba aliyewahi kucheza naye kwenye filamu yas ‘Misukosuko’.

J Plus amesema, “Nategemea hii filamu ya ‘The Foundation’ irudishe heshima ya filamu za action Tanzania kama ilivyo kuwa awali.”

Aidha kuna tetesi nyingi zilienea kuwa J Plus na Inspekta Seba wamekuwa hawapatani kutokana na wawili hao kutoshiriki kwa pamoja kwenye filamu kwa muda mrefu huku Inspekta Seba akiwa anatoa filamu mwenyewe.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post