» » » 'YANGA YAZUA HOFU CAF'

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Timu ya Yanga ya Tanzania Imekua gumzo kwa wapinzani wao wa Algeria, Ghana na Kongo baada ya timu hiyo kuzidi kuimarika kila idara.
Yanga iko tayari kwa ajili ya mechi za Kombe la Shirikisho baada ya kutuma majina ya wachezaji wanne.

Hassan Kessy na Juma Mahadhi ni kati ya majina yaliyotumwa na Yanga katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Caf) jijini Cairo, Misri.

Kessy amejiunga na Yanga baada ya mkataba wake na Simba kwisha na Mahadhi ametokea Coasta Union ya Tanga.

Pamoja na hayo, Yanga imeongeza majina mengine mawili ya kiungo wake Andrew Vicent 'Dante' kutoka Mtibwa Sugar na Beno Kakolanya ambaye amejiunga nao akitokea Prisons ya Mbeya.

Awali, Yanga ilipeleka majina 24 Caf, hivyo kuongezeka kwa majina hayo manne, maana yake ni majina 28 na inaendelea kubaki na nafasi mbili.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post