
Kocha
Athumani Bilali ‘Bilo’ amewaambia Yanga wanahitaji kupambana katika
mchezo wao wa kesho dhidi ya MO Bejaia kwani Watanzania wote wako nyuma
yao, hivyo wanahitaji kushinda mtanange huo ili kuwapa raha.
Yanga
kesho itakuwa na kibarua kikubwa nchini Algeria pale watakapowavaa
Waarabu hao katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika katika Kundi A.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Bilo ambaye ni kocha msaidizi wa Stand United
amesema Watanzania wapo pamoja na Yanga katika mchezo huo, hivyo
wanatakiwa kutambua wanahitaji ushindi.
