Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi amesema watu hao walikamatwa Juni mosi saa 12 jioni wakiwa na kilo mbili, misokoto 12 ya bangi na lita 10 za pombe aina ya gongo, kitendo ambacho ni uvunjwaji wa sheria na taratibu za nchi.
Msangi aliwataja waliokamatwa kuwa ni Leticia Elias (52) mkazi wa Igombe, Thomas Lipovitia (49) mkazi wa Kibagaja na Majani Manyego (38) ambaye alikutwa akiuza gongo.
“Watuhumiwa wote wako chini ya ulinzi kwa mahojiano na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka,” alisema.
