ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Aaron Ramsey
Wales ilijifurukuta na kuilaza Urusi mabao matatu kwa nunge katika mechi ya mwisho na muhimu ya makundi jana usiku.
Aaron Ramsey na Neil Taylor na Gareth Bale walifunga mabao hayo muhimu
na kuisaidia timu hiyo ya kocha Chris Coleman ikiwa imejihakikishia
nafasi katika mkumbo wa pili kwa mara ya pili katika historia yake.
Wales 3-0 Urusi
Wapinzani wao wa jadi England walimudu sare tasa dhidi ya Slovakia mjini
Saint-Etienne na kuhakikisha kuwa Wales wanafuzu kwa raundi ya pili ya
mashindano hayo kama vinara wa kundi B.
Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Wales sasa watachuana na mshindi wa tatu katika kundi C A ama D.
Aaron Ramsey na Gareth Bale
Wales na England zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Euro baada ya mechi zake za kundi B kukamilika.
Vijana wa Chris Coleman wamewabamiza Russia mabao 3 kwa 0 na huku
England ikija ya pili kwenye kundi baada ya kubanwa mbavu na Slovakia.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO