
Kilosa.Chama
cha Wakulima wa Miwa Bonde la Ruhende (RCGA), wilayani Kilosa
wameziomba mamlaka husika kutatua mgogoro wa muda mrefu wa chama hicho
ambao umesababisha viongozi waliokuwapo madarakani kuondolewa kwa tuhuma
za ubadhirifu.
Mwenyekiti
wa muda wa chama hicho Christopher Hembu amesema viongozi wa awali
waliondolewa katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Tundu,
wilayani humo Machi 3 uliohudhuriwa na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi
Mwigulu Nchemba.
Katika
mkutano huo wajumbe waliwatuhumu viongozi waliokuwamo madarakani kwa
ubadhirifu wa mali za chama na kusababisha migogoro ya wakulima na
kiwanda cha sukari kilombero hali inayozorotesha maendeleo ya chama.
Hembu
amesema katika mkutano huo waziri Nchemba aliwaagiza kupitia na
kurekebisha katiba ya chama kwani ilionekana ina upungufu baada ya
nafasi za uongozi kuondolewa ukomo hali ambayo pia inasababisha mgogoro.
