
Rais John Magufuli leo amemteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi.
Jaji Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla
ya uteuzi huo, Jaji Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto, mkoani Tanga. Uteuzi huu unaanza mara moja leo.
