Simanjiro.Watoto
wawili wa familia moja kwenye kitongoji cha Nadosoito wilayani hapa
wamefariki dunia na wengine wawili kunusurika baada ya kula maandazi
yanayosadikiwa kuwa na sumu.
Baada
ya kula maandazi na kusikia maumivu ya tumbo, walipewa dawa za kienyeji
za jamii ya wafugaji wa kimasai badala ya kupelekwa hospitalini.
Mkuu
wa Wilaya ya Simanjiro, Mahmoud Kambona amesema watoto hao walifariki
Juni 14 saa 10:00 jioni na kuwataja waliofariki dunia kuwa ni Jonas
Zebedayo (17) na John Zebedayo (14), huku Elizabeth Zebedayo (12) na
Joshua Zebedayo (11) waliosurika wakiwa wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya
Mount Meru wakitibiwa.
Amesema
chanzo cha vifo vivyo ni chakula chenye sumu walichokula wakati wazazi
wao hawapo nyumbani, lakini akasema wamechukua mabaki hayo na kupeleka
kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili uchunguzi ufanyike kubaini chanzo.
