» » Waethiopia 13 mbaroni kwa uhamiaji haramu

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Songwe. Polisi mkoani Songwe inawashikilia wahamiaji haramu 13 raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa wakiwa katika harakati za kutaka kuvuka mpaka kwenda Afrika Kusini.

 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ambwene Mwanyasi amesema wahamiaji hao walikamatwa juzi saa 12 jioni eneo la Mlowo wilayani Mbozi.

 Mwanyasi alisema wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa katika gari aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na mkazi wa Tunduma wilayani Momba na baada ya kuhojiwa walidai walikuwa wakienda Afrika Kusini kutafuta ajira.

 Ofisa Uhamiaji na Mwanasheria kutoka Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha Tunduma, Mashaka Manyamabunini amesema wahamiaji hao wamekiri kuwa lengo lao lilikuwa ni kupita Tanzania, huku akiwataka wananchi kuacha biashara ya usafirishaji wa binadamu.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post