Wakati siku chache zikiwa zimesalia kumalizika kwa vikao vya bunge la
11, wabunge wameendelea kusimama bungeni kuwasilisha mahitaji ya
wananchi wao majimboni. Nakukutanisha na mbunge wa Pangani Tanga Jumaa
Aweso ambaye anataka kufahamu zaidi ya milioni 200 zilizotengwa katika
jimbo lake hazijafika hadi sasa.
Aweso amesema…>>>’Mpaka sasa nionyeshe masikitiko yangu
kutokana na changamoto ya maji katika jimbo la Pangani, fedha zilizokuwa
zimeidhinishwa jumla ya shilingi milioni 200 hadi sasa hazijafika na
wakati bajeti inafikia ukingoni‘ –Jumaa Aweso
