» » UVCCM Wilaya ya Arusha mjini imefanya tafrija ya kumuaga katibu wake ngugu Jamal Khamji

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

katika hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbali Mbali wa chama na serikali pamoja na dini

wamemwelezea katibu Jamal khimji kama mtu aliyekuwa kiunganishi muhimu kwa wanaarusha hakuwa na makundi wala uchonganishi


Akizungumza kwaniaba ya vijana wa Arusha mwkt wa UVCCM Arusha mjini Ndg.Martin Munisi amemwelezea ktb khimji kama kiunganishi na aliyekuwa mchapa kazi ambaye hakuwa mwongo wala hakuwa mtu wa makundi alifanya kazi za jumuia kwa mujibu wa katiba na kanuni za UVCCM na CCM tunamtakia kila la kheri huko aendako

Mwkt wa CCM wilaya ya Arusha mjini Dr.Soileli amemtaka Khimji kwenda kuendeleza yale mema aliyo kuwa anayatenda Arusha

katibu wa UWT mkoa Fatma Hassan amemtaka ktb mgeni kumuiga khimji maana khimji alikuwa anawatetea machinga wa Arusha na wamama waliyo kuwa wananyanyaswa na mgambo wa jiji

naye katibu wa wazazi amemtaka khimji kwenda kutenda kama alivyo kuwa anatenda Arusha huku akimtaka katibu mgeni kuishi kwa amani kama alivyowakuta wanaarusha wakiishi kama ndugu bila mafarakano


akitoa neno la shukrani katibu jamali amewashukuru vijana wa Arusha kwa ushirikiano waliyo mpa na alipokuwa  akitekeleza majukumu yake yakila siku

katibu jamal anahamia Dodoma akimkabidhi ndugu Idd Mtopa aliyehama kutoka Kilosa na kuhamia Arusha mjini
         Imetolewa na

Afisa habari wilaya ya Arusha mjini S .Abdul
     leo tar 17.6.2016
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post