“Mbunge akisaini analipwa posho hiyo iko kwa mujibu wa kanuni, sasa yeye Dk Tulia juzi alipotoa mwongozo alianza na kanuni lakini baadaye akaingia kwenye taratibu tofauti, kwamba mbunge akisaini na kutoka hatalipwa, hapo amechemsha,” alisema Silinde.
Alisisitiza kuwa hatua hiyo ni kinyume na utaratibu, kwani kiongozi huyo wa Bunge alitoa hukumu ya kesi inayomhusu yeye mwenyewe.
“Malipo yawe kwa mtu anayechangia kwa kuwa kuna wabunge wanaingia na kusaini, lakini hawasemi chochote bungeni, kazi yao ni kupiga makofi tu na hawachangii,” alisema.
