» » TFF yagonga mwamba Yanga, yakubali yaishe

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO


Dar es Salaam. Hatimaye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesalimu amri kwa kukubalia  uchaguzi wa klabu hiyo ufanyike Juni 11 badala ya 25.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kuwa uamuzi huo umetokana na kikao kilichokutanisha pande hizo mbili na kufikia mwafaka.

TFF iliwakilishwa na Rais, Jamal Malinzi, Katibu Mkuu, Celestine Mwesigwa na Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Wanachama na Sheria, Eliud Mvela huku Yanga ikiwakilishwa na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.

 Lucas alisema kikao hicho kiliridhia mchakato huo wa uchaguzi uendelee huku Malinzi akiagiza kamati ya uchaguzi ya Yanga iwe msimamizi wa uchaguzi huo, huku kamati ya uchaguzi ya TFF ikiwa  mwangalizi.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Mashak

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post