ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO
Mbeya. Zaidi ya tani 1,150 za sukari zinatarajia kuingia mkoani Mbeya
kuanzia leo kutoka nchini Malawi kwa lengo la kupunguza uhaba wa bidhaa
hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipokuwa
akizungumza na wafanyabiashara wa mkoani hapa katika ukumbi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, kwa lengo la kusikiliza kero
zao.
Amesema tayari kuna magari 30 yapo njiani yanatokea nchini Malawi ambayo
kila moja lina tani 34 za sukari na muda wowote yataingia mkoani hapa.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO