» » Simba wakanusha kuuza vijana wao wa U20

ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

Kila mchezaji wa timu ya Simba ya umri wa miaka 20 aliyekwenda kwa mkopo timu zingine za ligi kuu Tanzania Bara, amekuwa akiwika na hata kuzungumziwa kwa nini anakosa nafasi kikosi cha kwanza.

Uongozi wa klabu ya Simba umekanusha kuwauza wachezaji wake walio kwa mkopo kwenye vilabu vingine, kama inavyopotoshwa na vyombo vingine vya habari.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema bado wachezaji hao wanamikataba na Simba, ila wapo kwenye vilabu hivyo kwa nia ya kupata uzoefu.

Poppe amesema wachezaji wa timu B, waliopelekwa kwa mkopo vilabu vingine, wanafatiliwa maendelea yao."Mfano kama yule kijana Mbaraka Yussuph, yupo Kagera Sugar, yule mchezaji yupo vizuri sana sasa hivi, na tulitaka kumrudisha, lakini yeye mwenyewe kaomba aendelee kupata uzoefu na sisi tumeona tumuongezee mkataba kwa sababu, tutamuhitaji baadae". amesema Poppe.
ILI UPATE HABARI ZETU KWA URAHISI BOFYA HAPA KUINSTAL APPLICATION YA MZALENDO HURU KWENYE SIMU YAKO

About Unknown

About Mzalendo Huru Staff:

Send us your articles, questions, feedback, suggestions, press releases and all others to Whats app on +255657905751
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post