Raia wanaofurahia mlo wa nyama ya mbwa nchini China
Sherehe ya kila mwaka ya kula mbwa imeanza kusini mwa taifa la China licha ya pinganizi kutoka katika taifa hilo na ugenini
Takriban mbwa 10,000 na paka wanatarajiwa kuuawa na kuliwa wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi inayofanyika Yulin.
Wanaharakati wanasema kuwa hafla hiyo ina ukatili huku wale wanaotaka sherehe hiyo kupigwa marufuku wakiandikisha saini milioni 11.
Mbwa
Je,sherehe hiyo inahusu nini?
Sherehe hiyo ya mlo wa nyama ya mbwa huwaleta pamoja watu wengi katika eneo la Yulin ili kujichagulia nyama ya mbwa, matunda na vinywaji.
Sherehe ya nyama ya mbwa Yulin


