Akiongea katika mkutano wa wawakilishi wa sekta ya usafiri wa anga wa nchi za SADC waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prof, Makame Mbarawa amesema licha ya kuwepo kwa umoja wa umoja wa kuangalia usalama wa nchi za SADC sasa pia serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiboresha sekta ya usafiri wa anga ikiwa pamoja na kuondoa baadhi ya kodi kwa mashirika ya ndege ili kuweza kuwapa unafuu watanzania katika usafiri wa anga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa SADC kwa upande wa sekta ya usafiri wa anga Bw, Geofrey Mashobesha amewataka wawakilishi wa jumuiya hiyo kujua ni njia gani zitakazo wezesha kuboresha sekta ya usafiri wa anga na kutatua changamoto na si kuishia kujadili pasipo utekelezaji.
Nae Mkurugenzi wa mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga Bw, Hamza Johari ameelezea changamoto zinazoikabili sekta ya anga hapa nchini ikiwemo ya uhaba wa marubani na wataalamu wa viwango vya kimataifa.
