Bw.Sadick ambaye pia ni mkuu wa mkoa ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko ya Bi Mariamu Halid aliyeambatana na mwanaye mwenye umri wa miaka saba ambaye alifanyiwa kitendo hicho kisha kutoa taarifa katika kituo cha polisi Himo bila msaada.
Amesema ni aibu kwa Jeshi la Polisi kufumbia macho vitendo vya ubakaji na ulawiti kwa watoto jambo ambalo linachangia ongezeko la matukio hayo huku jamii ikishindwa kutoa taarifa kwenye vyomba vya ulinzi na usalama.
Akizungumzia tukio hilo Bi Mariamu amesema licha ya wanakijiji kumkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha kituo kidogo cha polisi Himo tangu mwezi April mwaka huu hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yake huku mtoto huyo akiendelea kuteseka.
Baadhi ya wanaharakati wanaotetea na kusimamia haki za watoto wakiwa katika maadhisho ya siku ya mtoto wa Afrika wamesema matukio ya ubakaji na ulawiti yameshamiri huku taarifa za matukio hayo nyingi zikifanywa kuwa siri pamoja na Jeshi la polisi kushindwa kuwasaidia walalamikaji kutokana na uwepo wa mianya ya rushwa.
